Uponyaji na Ukombozi kwa Damu ya Yesu.

Friday, December 8, 2017

Share:

Sunday, November 26, 2017



MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
2Wafalme 4:18-37 “Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye wavunao. Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake. Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa………..” 
Watu wengi hapa Duniani wako katika mazingira haya inawezekena ukawa ni wewe, huyu mwanamke mshunami ambaye mtoto wake alikufa, alijitambu hivyo akasema kuwa hahitaji kulia. Alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu hivyo akajua kuwa Mungu anaweza kufanya jambo kwa ajili ya mtoto wake. 
Yule mtoto alikuwa amekufa lakini yule mwanamke alikataa kulia na kukubaliana na ile hali ya kifo cha mtoto wake, alijua wapi pa kwenda maana alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu. Ndipo alipochukua punda na mjakazi na kumwambia kuwa afanye haraka ili kuwahi kwa Mtumishi wa Mungu. Unapotaka kitu kitokee kwako fanya haraka kuwahi kwenye uwepo wa Mungu, maana Mungu wetu si mvivu hivyo unapaswa kufanya haraka ukitaka kitu kutoka kwake.

Share:
KUTOKA MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
Mathayo 14:22-27 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. ….. ”
Yesu akawaambi wanafunzi wake nendeni mbele kule ambako aliwaagiza waende, lakini katikati ya safari YESU akatokea kutoka kule mlimani alikokuwa akiomba peke yake. Siku unapotaka kuomba mbele za Mungu haijalishi ni watu wangapi wamekaa kando yako unapaswa kuwa peke yako, Mungu anapenda watu ambao wako peke yao. Wasahau wale walio kando yako na ujitazame wewe mwenyewe. Usimwangalie mume/mke wako, au ndugu yako aliye kaa jirani yako bali jiangalie mwenyewe na utamwona Mungu leo.
Yesu alitoka kule Mlimani akiwa tayari KUDHIHIRISHA NGUVU za MUNGU, huwezi kupata NGUVU za MUNGU mpaka uwe Mlimani na ukiwa peke yako. Tamani uwe peke yako ukiwa mbele za Mungu.
Baada ya maombi yale Yesu akatoka akiwa na UDHIHIRISHO wa NGUVU za MUNGU, unapotoka Mlimani unakuwa na uhakika wa NGUVU za MUNGU. Baada ya Yesu kufika kwa wanafunzi wake “akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Siku ya leo ninakwambia kuwa USIOGOPE maana kuna kitu kitakutokea katika maisha yako, jiandae kupokea muujiza wako.

Share:

Yeye yupo tayari kwa ajili yako, Je! Wewe uko tayari kwa ajili yake?

KUTOKA MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
Leo ni siku yako ya kubadilishwa;

Siku zote Mungu anaiangalia siku, kwa sababu yeye hayuko katika wakati wala majira, Mungu ni Mungu na matendo yake yanaelekezwa kwa siku, wewe ndio unaye tazamia wakati na majira lakini ndani yake hakuna majira, Yeye ni yule yule jana leo na hata milele. 
Hii inamaana gani? Inamaana jinsi alivyokuwa jana ndivyo hivyo hivyo alivyo leo, na kama alivyo leo ndivyo atakavyokuwa kesho, Mungu wetu habadiliki, wewe unaweza kubadilika lakini Yeye kamwe hata badilika. Wewe unaweza kubadilika na unatakiwa kubadilishwa ili kwamba uweze kutembea pamoja naye na ili uwe tayari kwa ajili yake.
Share:

SOMO: TOBA

KUTOKA MWENGE.
MCHUNGAJI ABIGAEL. 
Zaburi 51: 1-3 “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. ”
Yako mambo mengi ambayo wanadamu tunafanya ambayo hayampendezi Mungu lakini tunakuja mbele zake na kujifariji kana kwamba hakuna tulicho kosea badala ya kumlilia Mungu ili tuweze kupata huruma zake. Ukijua kuwa kuna jambo ambalo si zuri umelifanya usijifanye kama hujui bali unapaswa kutubu na kuacha.
Kanuni ya Mungu; Unapotenda dhambi au kukosea usimkimbie Mungu bali unapaswa kumkimbilia YEYE naye atakuosha na kukusafisha dhambi zako nawe utakuwa safi, usiwe na moyo mgumu, yatupasa kuacha uovu ili tuwe na furaha mbele za Mungu.
Ni mambo mangapi umefanya yasiyo mazuri mbele za Mungu na ukajifariji?, Hebu kubali kutubu na kuachana na uovu ulio kukamata ili uwe na FURAHA mbele za Bwana.
Lazima tukubali kuachana na dhambi ili tuweze kupokea kutoka kwa Mungu.
Lazia tutubu mbele za Mungu na si kujipaka mafuta wakati tu wachafu.
Share:
KUTOKA MWENGE.
MCHUNGAJI HELLEN MWINGA.
Marko 11:24 “ Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. ”
Chochote unacho omba ukisali, amini kuwa umepokea, unatakiwa umuombe Mungu na si mwanadamu, kuna mambo mengi tunayo tamani kupokea na hatuwezi kwa sababu hatujui nani wa kumuomba, wakati mwingine tumekuwa wepesi kuwaeleza watu shida zetu badala ya kumwambia Mungu. Unapaswa kuwa makini katika maombi yako ili uweze kupokea.
Neno la Mungu linasema ukiwa na imani unauwezo wa kuuambia mlima huu ng’oka na itakuwa hivyo, Mlima ni nini? Ni chochote kinacho kuzuia usipite au usisonge mbele, hivyo ukiwa na imani unauwezo wa kukiambia hicho kinachokuzuia kiondoke na ikawa hivyo

Share:

Sunday, November 19, 2017

Chini ya jua mwanadamu akikosa furaha, anakosa changamko la moyo.
Mwanadamu yeyote akipata furaha ambayo chanzo chake ni Kristo, atachangamka.
Yeyote aliyekosa furaha ana chuki, ni mtu wa kuchukiwa, atahuzunishwa na mke, na mume, na watoto.
Mtu mwenye furaha ya wokovu, hata akifiwa na mtu ampendae sana, akiwa na hakika afaye afa katika Bwana, atahuzunika kimwili tu, bali hatokuwa na huzuni katika moyo wake.
Mtu mwenye furaha ya wokovu hatasumbuliwa na maneno ya wakosaji.
Na Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni.

Share:

SHUHUDA.

Naitwa mtumishi Rose Nkondola wa eneo la Sayuni, namshukuru Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, 
Jambo la kwanza, ninamshukuru Mungu kwa ibada ya jumapili iliyopita, ilikuwa ni ibada ya furaha ya wokovu. Baada ya neno, mchungaji aliita wagonjwa japo sikuwa naumwa popote lakini nilipita mbele na mchungaji alipokuwa akiomba kwa uchungu nikaanza kufunguliwa, nikaanza kuomba msamaha kwa Mungu kwa yale mabaya niliyomtenda na kisha nguvu ya Mungu ikanishukia, nikahamishiwa katika ulimwengu wa roho nikaanza kumsifu na kumshukuru Mungu kwa kunirejeshea furaha tele ya wokovu na kunipa nguvu tele ya kutenda kazi yake.
Jambo la pili, nilikuwa nasumbuliwa na mguu toka mwaka 2011, ambapo ulianza baada ya kuona kama mtu ananichoma na sindano kwenye goti, nilipokuwa natoka shambani nilisumbuka nao sana. Katika bada ya Jumamosi kabla ya kwenda kusanyiko mwaka huu, Mchungaji aliyekuwepo siku hiyo, alisema kila anayeumwa aweke mkono pale anapoumwa,na atapokea uponyaji hapohapo au uponyaji utamfuata popote atakapokuwa, nami nikaweka mkono kwenye goti lile, kisha nilipokuwa nyumbani nimelala nikaota mtu amekuja ghafla akaingia ndani ya goti, akachomoa spoku na sindano, na toka hapo maumivu yameisha.
Namshukuru sana Mungu kwa huruma yake ameniponya bure, namshukuru sana.

Share:

Sunday, September 24, 2017

Vipo vizuizi vitano vinavyozuilia watu ulimwenguni kama

1. Kizuizi kinachohusika na uhuru wako
Umezaliwa ili uweze kufurahia baraka za Mungu na pia uweze kurithi vitu vyote vilivyomo katika ulimwengu huu.
Mwanadam amepungukiwa uwezo na nguvu wa kuweza kumiliki vitu vyote vilivyo katika ulimwengu huu ni lazima mwanadam akubali kulipa gharama ya kukipata alichotarajia au anachotarajia kukipata.
Wote waliookoka hutafutwa sana na shetani, ili kujiweka huru na salama ni lazima usimame imara kupigania haki pamoja na kuulinda muujiza ulioupata, maana unaposhindwa kuulinda muujiza ulioupata shetani atakupokonya au kuuharibu.
#ZINGATIA: Unapopata pata muujiza usimnyamazie Mungu, zidi kumsihi Mungu akupe neema ya kuutunza huo muujiza ulio upokea.
Amen....
Na Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni.

Share:

MUENDELEZO WA SOMO LILIPITA: KIZUIZI

MCHUNGAJI KIONGOZI PHILIPO JAMES GUNI
Kizuizi ni uzio au ukuta unaokuzulia kuyafikia mabadiliko yako katka maendeleo yako .
Wengi miongoni mwa waliookoka baraka zao zipo nje na wao wapo ndani.
Wengi waliookoka hawajafanikiwa kwa kumiliki baraka zao katika wokovu.
Vizuizi vinaweza kukuzuia katika sehemu tofauti tofauti kama maendeleo yako, biashara yako, afya yako ya kimwili na kiroho.
Share:

Friday, September 22, 2017


Kuna kitu kikubwa Bwana Yesu analazimika kukifanya kwako.Anataka kukupa amani na tumaini lililopotea kulirejesha upya. Kwake wewe ni wa thamani sana,tena anakupenda na kukuheshimu.Usipuuze ujumbe huu wengi wamepokea uponyaji kwa kuamini na kuupokea ujumbe tu Comment_nimepokea_kwa_jina_la_Yesu_kisha_like_share
Share:

Sunday, September 17, 2017

Haleluya watumishi wa Bwana, karibuni katika Ibada za Jumapili ya leo hapa Efatha Ministry na katika vituo vyetu vyote vya Efatha Ministry ndani na nje ya nchi.
Kama uko mbali usikose kufuatilia Ibada hizi kupitia ukurasa huu wa Facebook , TRENET TV na katika Internet
Kusikiliza: www.mixlr.com/efatha-ministry 
YouTube: https://youtu.be/jS0ZoZDsV6s
Share:

Matukio kabla ya ibada.

Wana wa Mungu wakimsubiri na kumpokea Mchungaji kiongozi philipo James Guni.



Share:

Saturday, September 9, 2017

KUKUBALI.


Unahitaji kusikia Neno la Kristo linalohubiriwa na Manabii, Mitume na Watumishi wote wa Mungu, na baada kusikia kuna hatua inayofuata nayo ni KUKUBALI.
2 Nyakati 20:20 “Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwamini Bwana, MUNGU wenu, ndivyo mtakavyothibitika waaminini MANABII wake, ndivyo mtakavyo fanikiwa.”
Unahitajika KUKUBALI yale yote yanayohusiana na Ufalme wa Mungu, kwa sababu Mungu ana mpango wa KUKUTHIBITISHA. Mafanikio hayaji kama Mungu HAJAYAPITISHA, Mibaraka haimfikii mtu yeyote tu isipokuwa yule ambaye Mungu amemuwekea MUHURI wake ya kwamba huyo ABARIKIWE.
Mimi na wewe tunapaswa kukubali ya kwamba yule aliyetuwekea Ahadi nyingi katika Maisha yetu anataka KUZITHIBITISHA kwetu lakini YEYE Atazithibitisha kwa yule ambaye AMESIKIA NENO lake na KUKUBALI kile alicho KISIKIA, mtu huyo ukawe ni wewe kwa jina la YESU, Amen; UKATHIBITISHE KUPITIA NENO HILI.
Kwa nini unatakiwa Kukubali Habari za Ufalme wa Mungu unao hubiriwa? Kwa sababu unahitajika kuyabeba Mafanikio ya Ufalme wa Mungu.
Katikati ya watu wanao mtambulisha Mungu huku duniani wenye kuyabeba MAFANIKIO ni watu wachache sana. Kwa nini? Kwa sababu wengine WAMESIKIA lakini wamegoma kukubaliana na kile ambacho WAMEKISIKIA, hivyo hawawezi kupokea AHADI ambazo Mungu ameziahidi katika Maisha yao.
MUNGU akakujalie wewe kukubali kwa sababu YEYE Amekupa kuyabeba MAFANIKIO katika UFALME wake.

 Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni, EFATHA MINISTRY- RUVUMA.

Share:

Sunday, September 3, 2017

Ukiwa katika kusubiria Muujiza wako lazima

1. Majaribu yaambatane nawe. Lazima uelewe wakati unasubiria muujiza wako majaribu ni lazima, usikwepe lazima ujaribiwe/upimwe je unaweza kupewa hicho ambacho unakisubiria.
Ukiwa katika kujaribiwa unapaswa kufanya yafuatayo:
-Kiri hicho ambacho unaamini.
Ayubu 23:10
2. Lazima utapitia mabaya.
Ukiona watu wanakutenga, wanakusema, hali ya msongo wa mawazo, hali ya kukata tamaa ujue upo katika msimu wa kusubiria muuijza wako.
3. Lazima utapitia kukatiswa tamaa.

unatakiwa kufanya nini ukiwa katika kusubiri?
1. Mwamini Mungu toka ndani ya moyo wako kuwa Mungu anaweza kufanya katika hilo unasubiria.

2. Soma neno la Mungu na kulishika.

3. Usiache kumkumbusha Bwana katika kile ambacho Mungu amekuahidi.
Isaya 62:6
Mtumishi wa Mungu Noel Michael Kapinga
Share:

MSIMU WA KUSUBIRI. (WAITING SEASON).

MSIMU WA KUSUBIRI. (WAITING SEASON).
Hauwezi kusubiri pasipo AHADI
Inaanza ahadi ndio panafuata kusubiri
Kuna msimu wa kupata na kuna msimu wa kusubiri, ukiwa katika kusubiri unahitaji
1. Uwe na tumaini.
2. Lazima uwe na Imani ukikosa Imani utakosa kile ambacho unasubiria, watu wengi wameshindwa kupokea ni kwa sababu ya kukosa Imani.
3. Lazima uwe mwaminifu.
Ukikosa uaminifu katika kusubiri Mungu anakasirika, na kile ambacho unakisubiria kinaondoka.
Kuwa mwaminifu katika muda, mali, fedha, katika hicho ambacho Mungu amekuandalia au amekupa.
4. lazima uwe na nguvu ya Mungu katika kusubiri.(Ayubu 6:11)
Lazima uwe na nguvu katika hicho ambacho unasubiri ili uujue mwisho wa kusubiria kwako sio unasema tu Mungu atafanya.
Wakati wa kusubiria muujiza wako au Baraka zako ndio wakati wa Mungu kukuandaa, tambua katika hicho ambacho unakisubiria kukipata, tambua kuwa Mungu anakuandaa ili uweze kukaa katika hiyo sehemu ambayo unaitarajia, kazi unayotarajia, biashara unayotarjia, kampuni unayotarajia.
Ndio maana bibi harusi anaandaliwa ili aweze kwenda kwenye harusi hawezi kuondoka katika ya kuandaliwa lazima asubiri mpaka fundi amalize ndipo aondoke, ndivyo hivyo hata kwa Mungu wengi wenu Mungu anawaandaa lakini kabla haujakamilishwa unakimbia, kukimbia kwako kunaondoa Baraka ulizoandaliwa.
MTUMISHI WA MUNGU NOEL MICHAEL KAPINGA.
Share:

Saturday, September 2, 2017

Welcome to the 9th Annual Gathering 2017. All guests both local and international.

Share:

Thursday, August 31, 2017

SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

NEEMA ni ya Bwana YESU, UPENDO ni wa Mungu BABA na USHIRIKA ni wa ROHO MTAKATIFU.
NEEMA ni Nini? Neema ni kitu ambacho mtu Anaweza kukipata pasipo kustahili. Tumeokolewa kwa Neema, sisi tulikuwa ni wenye dhambi na wala hatukustahili kuokolewa, lakini kwa Neema ya Bwana YESU tumepata kuokolewa.
Kwa nini Neema? Neema ndiyo inayokufungulia ili uweze kufika mahali ambapo utakuwa na SHUKRANI kwa Mungu, bila Neema huwezi kuwa na SHUKRANI. Kwa nini mtu mwenye Neema anakuwa na Shukrani? Ni kwa sababu ametendewa kitu ambacho hakutarajia kukipata. Jambo lolote ambalo unalipata pasipo tarajio na likakupa wewe Ahueni, Nafuu au Faraja hiyo ndiyo inaitwa NEEMA.
Neema ni ya muhimu sana kwa mtu yeyote yule Anayetamani kwenda mbele, awe ameokoka au hajaokoka, mtu akishafikiwa na Neema anakuwa na Changamko katika Maisha yake na SHUKRANI kwa Mungu wake, bila NEEMA hakuna Changamko wala Shukrani.
ITAMANI NEEMA KATIKA MAISHA YAKO ILI UWEZE KUWA BORA.
:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.
Share:

NEEMA

Kazi ya Neema ni kuondoa HUZUNI na MACHUNGU, usione mtu ana HUZUNI au MACHUNGU ukajua kuwa hana UPENDO, La! Anao lakini kuna kitu kimekosekana kwake ambacho ni NEEMA; akipata NEEMA changamko linatokea katika Maisha yake.
• NEEMA ikikosekana kwako maswali yanakuwa mengi juu yako, Mtu mwenye NEEMA huwa hakataliwi popote pale atakapokwenda.
• Ili uweze Kuchanua unahitaji NEEMA, ukiwa mwanaume ni lazima NEEMA izidi kwako ili uweze kusababisha jambo litokee katika Maisha na Familia yako kiujumla.
• NEEMA ndiyo inayokuhalalisha wewe uweze Kukubalika, pasipo NEEMA huwezi kukubalika mbele za Mungu wala wanadamu, hata ungefanya jambo JEMA au ZURI kiasi gani.
• Ukiwa mahali ambapo umekwama kabisa NEEMA ndipo inapojitokeza na kukupa Msaada, NEEMA ndiyo inayoleta usaidizi, ili uweze kusaidiwa unahitaji NEEMA.
• Ukikosa NEEMA hata kama una sura nzuri hakuna atakayekuhitaji Kukuoa au atakayekubali kuolewa na wewe, NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha yako.

Ukiwa na NEEMA ndipo UBORA wako unapoanza Kuonekana, pasipo NEEMA huwezi kuwa BORA. NEEMA ni ya MUHIMU sana kwa kila mtu ambaye yuko chini ya jua, ili aweze kutokeza mahali na aonekane kuwa Yeye ni mtu. Ukiwa na UPENDO na NEEMA unaweza kufanya jambo na UKAFANIKIWA, lakini ukiwa na UPENDO bila NEEMA hakuna kitu ambacho utakifanya na KIKAFANIKIWA.
NEEMA ni ya MUHIMU sana kwa kila anayetamani kwenda Mbele au Kufanikiwa.
:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.
Share:

UHALISIA.

UHALISIA
Katika kuishi kwako tambua kuna watu wamepewa vipawa,karama na vipaji ,Mungu ndie kawa gawia,
Sasa basi ukiwabaini unatakiwa uwa tunze,uwafundishe na kuwaongoza kwa upendo na hekima ,na wao wafurahi kuongozwa na wewe, ili uje kuvuna matunda mema baadae, sio kuwakatisha tamaa,kumbuka Mungu amekukutanisha nao kwa kusudi, unajua mara nyingine sio rahisi wewe kujua kila kitu,wengi hapo ndio tunakwama.
Tuwafanye watu kufanya wanachotakiwa kufanya,tuwafanye watu kuwa wanavyotakiwa kuwa,waamini .
Barikiwa
Mtumishi wa Mungu Noely Kapinga.
Share:

Sunday, August 27, 2017

SHUHUDA
Naitwa Avelina Haule

Namshukuru Mungu sana sana, nilikuwa nasumbuliwa na magonjwa mengi mengi kama #kisukari, #presha, na #malaria sugu ambayo kila dawa ilikuwa ikidunda tangu mpaka mwaka 1999, nilikuwa mtu wa kungangania dini kwa kipindi chote huku nikizunguka huku na kule kwa waganga wa kienyeji, hospitali kwenye matambiko lakini sikupata neema ya kupona kwa kipindi chote hicho lakini namshukuru huyu Mungu tangu nimeingia hapa Efatha navuta pumzi nzuri sina ugonjwa tena maana ilifika mahali mpaka napelekwa hospital napumulia mashine na wakati mwingine hata kutembea nilikuwa siwezi lakini namshukuru huyo Mungu mimi sasa ni mzima na nimeachana na dini na kuachana na wenyekiti wa jumuiy
a niliyokuwa nikitumikia kwa muda wa miaka 15. 
Share:

Sunday, August 20, 2017

Sunday Service.

Sunday Service.
Walokole wengi wavivu kupokea,huwezi kupata mafanikio kwa njia ya kufunga na kuomba. Hautakaa ufanikiwe katika hicho ambacho ulipewa upokee kwa kuwekewa mikono na wapakwa mafuta wa Bwana isipokuwa kwa kukichochea hicho kipawa.
Neema ya Mungu ni kwaajili ya watoto wa wachanga wa Imani ya Kristo,
Neema ni haki ya walokole wote. Neema naweza kufananisha na mahitaji ya kila siku ambayo mzazi ama mlezi anahusika kutoa kwa watoto wake. Hapo nyuma kipindi Israeli inatembea kutoka Misri kwenda nchi ya Ahadi kwa muda wa miaka kumi walikuwa wakila chakula kutoka mbinguni kinachoitwa Mana. (Neema kwa kipindi kile tunaweza sema kama mana). Neema ni kwaajili ya kila mtu hapa chini ya jua.
Mtumishi wa Mungu Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni.
Share:

USHUHUDA

Naitwa Noel Athuman
Namshukuru Mungu kupitia semina ya kitume na kinabii nimetendewa mambo mengi kupitia neno la mtumishi wa Mungu aliyesimama mara ya mwisho katika semina alitutangazia kuwa wiki linalofuata baada ya wiki hile ya semina tutapokea zawadi.
 Namshukuru Mungu nimepata zawadi ya mtaji maana ilifika mahali mtaji ulikuwa unaelekea kuisha.

Pia, Namshukuru Mungu kanipa zadi ya shamba na mbegu zake katika hilo shamba na pia kupitia neno hilohilo namshukuru Mungu nimepa kazi tatu kwa wakati mmoja. Pia namshukuru zipo zawadi nyingi nimepata siwezi kusema zote ila namshukuru Mungu katika hayo. 
Share:

Sunday, August 13, 2017

SENIOR PASTOR PHILIPO JAMES GUNI 

REWARD.

Reward is anything that people gives as part of identification or part of testifying on what he/she has minister.
It’s to give something to someone due to what he/she has done.
Philippian 3:13-14
If there is a person who is giving you a gift
 He has valued you and appreciated you.
It’s a sign and wonder’s that he/she respect you because you have done than others.
 You're identified for what you've done.

Share:

Sunday Service.

MCH. KIONGOZI PHILIPO JAMES GUNI.
THAWABU.
Thawabu ni kitu chochote ambacho mtu anapewa kama sehemu ya utambulisho au sehemu ya uthibitisho wa huduma aliyoitoa.
Ni kitu chochote apewacho mtu kutokana na kazi aliyoifanya.
Filipi 3:13-14.
Mtu anayetoa thawabu ni ishara ya kuonyesha
- Amekuheshimu au kukuthamini.
unaheshimika kwasababu umefanya zaidi ya wengine.
- Unatambulika kwa kile ambacho umefanya.
Share:

Friday, August 11, 2017

SOMO: USTAWI WA MWAMINI.

 
MCH KIONGOZI MKOA WA MWANZA : VICTOR MALAMLA.
SOMO: USTAWI WA MWAMINI.


Waraka wa tatu wa Yohana 1:2 
Mungu anataka kila mwamini astawi, Ustawi ni utoshelevu wa kila unachohitaji, au ni ile hali yakufanikiwa kibiashara , kiofisi, familia nk.
Ustawi ni ile hali yakuushinda umaskini, maana umaskini ni mateso tuupinge umaskini kwa nguvu zote, msimamizi wa umaskini ni shetani mwenyewe.
Laana ya umaskini ikimwandama mtu kumtoka ni kazi sana, kama roho ya umaskini haijashughulikiwa kwako kufanikiwa ni ndoto hata kama umeokoka. halooo


Share:

Sunday service





Huwezi kustawi kama sio mwaminifu katika matakatifu ya Mungu.
Matakatifu ya Mungu ni yapi?
Muda wote uliotengwa kwaajili ya Mungu.
Matoleo yako kwa Mungu.
Ahadi zako kwa Mungu.


Share:

Facebook

Kuhusu Efatha

EFATHA.
EFATHA
maana yake ni Funguka [MARKO 7:34], Efatha ni huduma iliyo chini ya Mtume na Nabii JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA,Huduma ilianzishwa mwaka 1997.

Huduma ya Efatha mkoa wa Ruvuma inaongozwa na Mchungaji kiongozi PHILIPO JAMES GUNI, Katika Mkoa wa Ruvuma Huduma ya Efatha inapatikana Songea eneo la Mkuzo na Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.
Huduma ya Efatha Ruvuma chini ya Mchungaji kiongozi PHILIPO JAMES GUNI,Tunatoa Huduma ya Uponyaji na Ukombozi kwa damu ya Yesu, Uponyaji na Ukombozi katika Magonjwa,Kipato, Kazi, Mazingira, Utasa, Ugumba, Uchumi ulioyumba, Umaskini, Ndoa, Kuachwa, Kuachika, Kukataliwa na mengine yote yaliyoshindikana, Huduma inatolewa bureee kwa damu ya YESU.
RATIBA ZETU ZA IBADA NI KAMA IFUATAVYO:
1.JUMATATU-IJUMAA –NI USHAURI NA MAOMBEZ, I Muda wote.
2.JUMAMOSI-IBADA YA MAOMBI, kuanzia saa 3:00 asubuhi-saa 6;00 mchana
3.JUMAPILI-IBADA KWA WATU WOTE, kuanzia saa 4:00 asubuhi- saa 8:00 mchana
Tunapatikana SONGEA-MKUZO, Kufika panda magari yaendayo MKUZO/MWENGEMSHINDO yanayopaki stendi kuu ya daladala Songea, shuka kituo kinachoitwa EFATHA uliza kanisa lililopo sio mbali kutoka barabarani.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Archive

Labels