Uponyaji na Ukombozi kwa Damu ya Yesu.

Sunday, November 26, 2017



MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
2Wafalme 4:18-37 “Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye wavunao. Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake. Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa………..” 
Watu wengi hapa Duniani wako katika mazingira haya inawezekena ukawa ni wewe, huyu mwanamke mshunami ambaye mtoto wake alikufa, alijitambu hivyo akasema kuwa hahitaji kulia. Alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu hivyo akajua kuwa Mungu anaweza kufanya jambo kwa ajili ya mtoto wake. 
Yule mtoto alikuwa amekufa lakini yule mwanamke alikataa kulia na kukubaliana na ile hali ya kifo cha mtoto wake, alijua wapi pa kwenda maana alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu. Ndipo alipochukua punda na mjakazi na kumwambia kuwa afanye haraka ili kuwahi kwa Mtumishi wa Mungu. Unapotaka kitu kitokee kwako fanya haraka kuwahi kwenye uwepo wa Mungu, maana Mungu wetu si mvivu hivyo unapaswa kufanya haraka ukitaka kitu kutoka kwake.

Share:
KUTOKA MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
Mathayo 14:22-27 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. ….. ”
Yesu akawaambi wanafunzi wake nendeni mbele kule ambako aliwaagiza waende, lakini katikati ya safari YESU akatokea kutoka kule mlimani alikokuwa akiomba peke yake. Siku unapotaka kuomba mbele za Mungu haijalishi ni watu wangapi wamekaa kando yako unapaswa kuwa peke yako, Mungu anapenda watu ambao wako peke yao. Wasahau wale walio kando yako na ujitazame wewe mwenyewe. Usimwangalie mume/mke wako, au ndugu yako aliye kaa jirani yako bali jiangalie mwenyewe na utamwona Mungu leo.
Yesu alitoka kule Mlimani akiwa tayari KUDHIHIRISHA NGUVU za MUNGU, huwezi kupata NGUVU za MUNGU mpaka uwe Mlimani na ukiwa peke yako. Tamani uwe peke yako ukiwa mbele za Mungu.
Baada ya maombi yale Yesu akatoka akiwa na UDHIHIRISHO wa NGUVU za MUNGU, unapotoka Mlimani unakuwa na uhakika wa NGUVU za MUNGU. Baada ya Yesu kufika kwa wanafunzi wake “akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Siku ya leo ninakwambia kuwa USIOGOPE maana kuna kitu kitakutokea katika maisha yako, jiandae kupokea muujiza wako.

Share:

Yeye yupo tayari kwa ajili yako, Je! Wewe uko tayari kwa ajili yake?

KUTOKA MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
Leo ni siku yako ya kubadilishwa;

Siku zote Mungu anaiangalia siku, kwa sababu yeye hayuko katika wakati wala majira, Mungu ni Mungu na matendo yake yanaelekezwa kwa siku, wewe ndio unaye tazamia wakati na majira lakini ndani yake hakuna majira, Yeye ni yule yule jana leo na hata milele. 
Hii inamaana gani? Inamaana jinsi alivyokuwa jana ndivyo hivyo hivyo alivyo leo, na kama alivyo leo ndivyo atakavyokuwa kesho, Mungu wetu habadiliki, wewe unaweza kubadilika lakini Yeye kamwe hata badilika. Wewe unaweza kubadilika na unatakiwa kubadilishwa ili kwamba uweze kutembea pamoja naye na ili uwe tayari kwa ajili yake.
Share:

SOMO: TOBA

KUTOKA MWENGE.
MCHUNGAJI ABIGAEL. 
Zaburi 51: 1-3 “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. ”
Yako mambo mengi ambayo wanadamu tunafanya ambayo hayampendezi Mungu lakini tunakuja mbele zake na kujifariji kana kwamba hakuna tulicho kosea badala ya kumlilia Mungu ili tuweze kupata huruma zake. Ukijua kuwa kuna jambo ambalo si zuri umelifanya usijifanye kama hujui bali unapaswa kutubu na kuacha.
Kanuni ya Mungu; Unapotenda dhambi au kukosea usimkimbie Mungu bali unapaswa kumkimbilia YEYE naye atakuosha na kukusafisha dhambi zako nawe utakuwa safi, usiwe na moyo mgumu, yatupasa kuacha uovu ili tuwe na furaha mbele za Mungu.
Ni mambo mangapi umefanya yasiyo mazuri mbele za Mungu na ukajifariji?, Hebu kubali kutubu na kuachana na uovu ulio kukamata ili uwe na FURAHA mbele za Bwana.
Lazima tukubali kuachana na dhambi ili tuweze kupokea kutoka kwa Mungu.
Lazia tutubu mbele za Mungu na si kujipaka mafuta wakati tu wachafu.
Share:
KUTOKA MWENGE.
MCHUNGAJI HELLEN MWINGA.
Marko 11:24 “ Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. ”
Chochote unacho omba ukisali, amini kuwa umepokea, unatakiwa umuombe Mungu na si mwanadamu, kuna mambo mengi tunayo tamani kupokea na hatuwezi kwa sababu hatujui nani wa kumuomba, wakati mwingine tumekuwa wepesi kuwaeleza watu shida zetu badala ya kumwambia Mungu. Unapaswa kuwa makini katika maombi yako ili uweze kupokea.
Neno la Mungu linasema ukiwa na imani unauwezo wa kuuambia mlima huu ng’oka na itakuwa hivyo, Mlima ni nini? Ni chochote kinacho kuzuia usipite au usisonge mbele, hivyo ukiwa na imani unauwezo wa kukiambia hicho kinachokuzuia kiondoke na ikawa hivyo

Share:

Sunday, November 19, 2017

Chini ya jua mwanadamu akikosa furaha, anakosa changamko la moyo.
Mwanadamu yeyote akipata furaha ambayo chanzo chake ni Kristo, atachangamka.
Yeyote aliyekosa furaha ana chuki, ni mtu wa kuchukiwa, atahuzunishwa na mke, na mume, na watoto.
Mtu mwenye furaha ya wokovu, hata akifiwa na mtu ampendae sana, akiwa na hakika afaye afa katika Bwana, atahuzunika kimwili tu, bali hatokuwa na huzuni katika moyo wake.
Mtu mwenye furaha ya wokovu hatasumbuliwa na maneno ya wakosaji.
Na Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni.

Share:

SHUHUDA.

Naitwa mtumishi Rose Nkondola wa eneo la Sayuni, namshukuru Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, 
Jambo la kwanza, ninamshukuru Mungu kwa ibada ya jumapili iliyopita, ilikuwa ni ibada ya furaha ya wokovu. Baada ya neno, mchungaji aliita wagonjwa japo sikuwa naumwa popote lakini nilipita mbele na mchungaji alipokuwa akiomba kwa uchungu nikaanza kufunguliwa, nikaanza kuomba msamaha kwa Mungu kwa yale mabaya niliyomtenda na kisha nguvu ya Mungu ikanishukia, nikahamishiwa katika ulimwengu wa roho nikaanza kumsifu na kumshukuru Mungu kwa kunirejeshea furaha tele ya wokovu na kunipa nguvu tele ya kutenda kazi yake.
Jambo la pili, nilikuwa nasumbuliwa na mguu toka mwaka 2011, ambapo ulianza baada ya kuona kama mtu ananichoma na sindano kwenye goti, nilipokuwa natoka shambani nilisumbuka nao sana. Katika bada ya Jumamosi kabla ya kwenda kusanyiko mwaka huu, Mchungaji aliyekuwepo siku hiyo, alisema kila anayeumwa aweke mkono pale anapoumwa,na atapokea uponyaji hapohapo au uponyaji utamfuata popote atakapokuwa, nami nikaweka mkono kwenye goti lile, kisha nilipokuwa nyumbani nimelala nikaota mtu amekuja ghafla akaingia ndani ya goti, akachomoa spoku na sindano, na toka hapo maumivu yameisha.
Namshukuru sana Mungu kwa huruma yake ameniponya bure, namshukuru sana.

Share:

Facebook

Kuhusu Efatha

EFATHA.
EFATHA
maana yake ni Funguka [MARKO 7:34], Efatha ni huduma iliyo chini ya Mtume na Nabii JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA,Huduma ilianzishwa mwaka 1997.

Huduma ya Efatha mkoa wa Ruvuma inaongozwa na Mchungaji kiongozi PHILIPO JAMES GUNI, Katika Mkoa wa Ruvuma Huduma ya Efatha inapatikana Songea eneo la Mkuzo na Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.
Huduma ya Efatha Ruvuma chini ya Mchungaji kiongozi PHILIPO JAMES GUNI,Tunatoa Huduma ya Uponyaji na Ukombozi kwa damu ya Yesu, Uponyaji na Ukombozi katika Magonjwa,Kipato, Kazi, Mazingira, Utasa, Ugumba, Uchumi ulioyumba, Umaskini, Ndoa, Kuachwa, Kuachika, Kukataliwa na mengine yote yaliyoshindikana, Huduma inatolewa bureee kwa damu ya YESU.
RATIBA ZETU ZA IBADA NI KAMA IFUATAVYO:
1.JUMATATU-IJUMAA –NI USHAURI NA MAOMBEZ, I Muda wote.
2.JUMAMOSI-IBADA YA MAOMBI, kuanzia saa 3:00 asubuhi-saa 6;00 mchana
3.JUMAPILI-IBADA KWA WATU WOTE, kuanzia saa 4:00 asubuhi- saa 8:00 mchana
Tunapatikana SONGEA-MKUZO, Kufika panda magari yaendayo MKUZO/MWENGEMSHINDO yanayopaki stendi kuu ya daladala Songea, shuka kituo kinachoitwa EFATHA uliza kanisa lililopo sio mbali kutoka barabarani.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Archive

Labels