Naitwa Noel Athuman
Namshukuru Mungu kupitia semina ya kitume
na kinabii nimetendewa mambo mengi kupitia neno la mtumishi wa Mungu
aliyesimama mara ya mwisho katika semina alitutangazia kuwa wiki linalofuata
baada ya wiki hile ya semina tutapokea zawadi.
Namshukuru Mungu nimepata zawadi ya mtaji
maana ilifika mahali mtaji ulikuwa unaelekea kuisha.
Pia, Namshukuru
Mungu kanipa zadi ya shamba na mbegu zake katika hilo shamba na pia kupitia neno
hilohilo namshukuru Mungu nimepa kazi tatu kwa wakati mmoja. Pia namshukuru
zipo zawadi nyingi nimepata siwezi kusema zote ila namshukuru Mungu katika
hayo.
0 comments:
Post a Comment