SHUHUDA
Naitwa Avelina Haule
Namshukuru Mungu sana sana, nilikuwa
nasumbuliwa na magonjwa mengi mengi kama #kisukari, #presha, na #malaria sugu
ambayo kila dawa ilikuwa ikidunda tangu mpaka mwaka 1999, nilikuwa mtu wa
kungangania dini kwa kipindi chote huku nikizunguka huku na kule kwa waganga wa
kienyeji, hospitali kwenye matambiko lakini sikupata neema ya kupona kwa
kipindi chote hicho lakini namshukuru huyu Mungu tangu nimeingia hapa Efatha
navuta pumzi nzuri sina ugonjwa tena maana ilifika mahali mpaka napelekwa
hospital napumulia mashine na wakati mwingine hata kutembea nilikuwa siwezi
lakini namshukuru huyo Mungu mimi sasa ni mzima na nimeachana na dini na
kuachana na wenyekiti wa jumuiy
a niliyokuwa nikitumikia kwa muda wa miaka 15.
0 comments:
Post a Comment