• NEEMA ikikosekana kwako maswali yanakuwa mengi juu yako, Mtu mwenye NEEMA huwa hakataliwi popote pale atakapokwenda.
• Ili uweze Kuchanua unahitaji NEEMA, ukiwa mwanaume ni lazima NEEMA izidi kwako ili uweze kusababisha jambo litokee katika Maisha na Familia yako kiujumla.
• NEEMA ndiyo inayokuhalalisha wewe uweze Kukubalika, pasipo NEEMA huwezi kukubalika mbele za Mungu wala wanadamu, hata ungefanya jambo JEMA au ZURI kiasi gani.
• Ukiwa mahali ambapo umekwama kabisa NEEMA ndipo inapojitokeza na kukupa Msaada, NEEMA ndiyo inayoleta usaidizi, ili uweze kusaidiwa unahitaji NEEMA.
• Ukikosa NEEMA hata kama una sura nzuri hakuna atakayekuhitaji Kukuoa au atakayekubali kuolewa na wewe, NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha yako.
Ukiwa na NEEMA ndipo
UBORA wako unapoanza Kuonekana, pasipo NEEMA huwezi kuwa BORA. NEEMA ni
ya MUHIMU sana kwa kila mtu ambaye yuko chini ya jua, ili aweze kutokeza
mahali na aonekane kuwa Yeye ni mtu. Ukiwa na UPENDO na NEEMA unaweza
kufanya jambo na UKAFANIKIWA, lakini ukiwa na UPENDO bila NEEMA hakuna
kitu ambacho utakifanya na KIKAFANIKIWA.
NEEMA ni ya MUHIMU sana kwa kila anayetamani kwenda Mbele au Kufanikiwa.
:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.
NEEMA ni ya MUHIMU sana kwa kila anayetamani kwenda Mbele au Kufanikiwa.
:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.
0 comments:
Post a Comment